Baada ya mashindano ya miss
Tanzania 2016 kumalizika hivi karibuni ambapo Fainali zake zilifanyika
kwenye jiji la Mwanza kwa mara ya kwanza toka kuanzishwa kwa mashindano
hayo miaka zaidi ya ishirini iliyopita, Miss Tanzania 2016, Diana
Lukumai aliitangazwa mshindi wa taji hilo.
Licha ya kutokuwa mmoja ya washiriki
walioingia top ten, mrembo ambaye ni Miss Kilimanjaro, Glory Minja Leo
November 3 2016 amesaini rasmi mkataba wa mwaka mmoja kuwa balozi wa
Kampuni ya Teknolojia ya Magari ‘PII’.
Akizungumza kuhusu mkataba huo, Mkurugenzi wa Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Teknolojia ya Magari ‘PII’, Ebenezer Msuya
amesema kampuni yao imeingia mkataba na Glory kutokana na uwezo ambao
ameonyesha kwa kipindi ambacho walikuwa wakidhamini mashindano ya Miss
Tanzania na baada ya kutambua uwezo wa washiriki hao walibaini kuwa
Glory ana uwezo wa kufanya nao kazi.
>>>’Tumesaini
naye mkataba wa kufanya kazi, leo tumemkabidhi cheque ya milioni lakini
vilevile tumesaini naye mkataba wa mwaka mmoja ambao tutakuwa tunafanya
nae shughuli za kijamii pamoja na shughuli nyingine za kimasoko’;- Msuya.
kulikuwa na vigezo walikuwa wanavihitaji
mimi binafsi kuna vitu nilivifanya, walitupatia business card kwa kuwa
walijua tutazunguka mikoa
0 Reviews:
Write A Review